ZAIDI YA EKARI TATU ZA BANGI ZACHOMWA MOTO MAISOME , WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA.
MWANZA.
Zaidi ya Ekari tatu za bangi zimeteketezwa ndani ya hifadhi
ya msitu wa Maisome katka kisiwa cha
Maisome wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya
Sengerema Bw. Anne Mhina ambapo amesema zao hilo limelimwa katika sehemu ya
Msitu huo wenye ukubwa wa hekta elfu kumi na mbili na mia nane.
Aidha, amesema kuwa bangi hiyo imeteketezwa na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo katika operesheni maalumu ya
kukomesha kilimo cha zao hilo haramu.
Pia, amesema kuwa mikakati yao ni kukomesha kilimo
hicho,na kuwatafuta wanaolima zao hilo pamoja na mashamaba ya wakulima
yaliyooteshwa zao hilo ili kuyavuna na kuyateketeza.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala Misitu Tanzania TFS
wilaya ya Sengerema Bw. Urio Jeremaya amesesma kuwa mbali na hilo operesheni
hiyo imelenga kukomesha shughuli nyingine za kibinadamu zinazotishia uhai wa
hifadhi hiyo.
ZAIDI YA EKARI TATU ZA BANGI ZACHOMWA MOTO MAISOME , WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA.
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:
No comments