NDEGE YA ABIRIA 67 IMEANGUKA WAKATI IKITUA INCHINI NEPAL.


KATHMANDU.
Ndege ya abiria kutoka Bangladesh iliyokuwa na abiria 67 imeanguka wakati ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kathmandu nchini Nepal nakuua watu kadhaa.
Maafisa nchini Nepal wanasema kuwa abiria 17 kati ya 67 ndio waliookolewa huku wengine wakisadikiwa kupoteza maisha.
Habari zinaeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiitokea jijini Dhaka, kuelekea jijini Kathmandu.
Moto mkubwa na moshi mzito ulishuhudiwa wakati ndege hiyo ilipoanguka ambapo maafisa wamekuwa wakiendelea na  zoezi la kuuzima ili kuona iwapo wataweza  kuwaokoa abiria wengine.
Hata hivyo uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Marekani, US-Bangla.

NDEGE YA ABIRIA 67 IMEANGUKA WAKATI IKITUA INCHINI NEPAL. NDEGE YA ABIRIA 67 IMEANGUKA WAKATI IKITUA INCHINI NEPAL. Reviewed by safina radio on March 12, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.