OLF LIMEKUWA TISHIO KWA JESHI LA ETHIOPIA .
ADDIS ABABA.
Jeshi la Ethiopia limeanzisha uchunguzi kubaini namna raia
9 walivyouawa na wengine 12 kujeruhiwa baada ya kushambuliwa kimakosa
katika eneo la Moyale katika mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
Ripoti zinasema kuwa wanajeshi kadhaa wamesimishwa kazi, baada
ya kuwaua raia hao wakati wa makabiliano na waasi.
Jeshi la Ethiopia kwa muda mrefu sasa, limekuwa likipambana na
waasi wanaojiita Oromo Liberation Front (OLF) ambao serikali ya Addis Ababa
inasema ni magaidi na wanatishia usalama wa nchi hiyo.
Ethiopia imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama tangu
mwaka 2016, baada ya maandamano kutoka majimbo ya Oromia na Amhara.
Wakaazi wa majimbo hayo mawili, yanaishtumu serikali ya Ethiopia
kwa kuwatenga kimaendeleo hali iliyomsababisha Waziri Mkuu Hailemariam
Desalegn, kujiuzulu huku hali ya hatari ikitangazwa kwa muda wa miezi sita.
OLF LIMEKUWA TISHIO KWA JESHI LA ETHIOPIA .
Reviewed by safina radio
on
March 12, 2018
Rating:
No comments