DK. KIJAJI ATOA SIKU TATU KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA KUEZEKA MAJENGO MAWILI YA MADARASA YA SHULE YA SEKONDARI YA BUMBUTA.
Nainbu wazri wa fedha na mipango Dk. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa halmashauri
ya wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kuezeka majengo mawili ya vyumba vya madarasa
ya shule ya mpya ya Sekondari ya Bumbuta iliyojengwa na wananchi kwa kujitolea
kuwa nguvu kazi na rasilimali fedha.
![]() |
Nainbu wazri wa fedha na mipango Dk. Ashatu Kijaji. |
Ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua ujenzi wa
shule hiyo na kupata malalmiko kwa wananchi kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imekataa
kutumia sehemu ya fedha kiasi cha shilingi milioni 144 zilizotolewa na serikali
kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo vya shule hiyo.
Aidha, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano
inathamini nguvu ya mwananchi na kuwa fedha hizo za serikali zilitolewa kwa
wananchi wa Bumbuta kutokana na wananchi hao kuonyesha mfano wa kuigwa katika
kutekeleza shughuli za kimaendeleo.
Pia, Naibu Waziri Kijaji amesema kuwa serikali
imetambua mchango wa wananchi hao katika ujenzi huo wa vyumba vya madarasa hayo
kwa kutoa kiasi hicho cha fedha huku akionyesha kutoridhishwa kwa halmashauri
hiyo kutokumalizia ujenzi huo.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa shule hiyo
ya Sekondari ya Bumbuta Hashim Mshena amesema kuwa wananchi wamejenga madarasa
mawili kwa kujitolea lakini walipowasilisha maombi yao wilayani ya kutaka ujenzi
wa madarasa hayo yaezekwe kwa sehemu ya fedha ya milioni 144 zilizotolewa na
serikali maombi yao yalikataliwa.
DK. KIJAJI ATOA SIKU TATU KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KONDOA KUEZEKA MAJENGO MAWILI YA MADARASA YA SHULE YA SEKONDARI YA BUMBUTA.
Reviewed by safina radio
on
March 13, 2018
Rating:

No comments