WATOTO 2000 KATI YA 20,000 WAZALIWA WAKIWA NA TATIZO LA MOYO NCHINI.
Watoto elfu mbili pekee kati elfu ishiri waliozaliwa
wakiwa na tatizo la moyo nchini mwaka jana ndio waliofikishwa hospitalini kwa
ajili ya uchunguzi na matibabu.
![]() |
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Godwin Sharau (kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. |
Akizungumza katika Mkutano wa kujadili namna ya kudhibiti
ongezeko la ugonjwa wa moyo kwa watoto jijini Dar es salaam Daktari Bingwa wa
upasuaji wa magonjwa ya moyo katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete Dk. Godwin Sharau amesema kuwa watoto mia nne hamsini kati ya elfu
mbili wamepatiwa matibabu.
Dk. Sharau amesema kuwa sababu za ongezeko la
ugonjwa huo ni kutokana na mfumo wa maisha ambao umekuwa ukichangia kuongezeka
kwa ugonjwa huo kwa watoto.
Aidha, jumla ya madaktari kumi na moja kutoka Tanzania
wamepatiwa ujuzi wa kudhibiti ugonjwa wa moyo kutoka Hospitali ya Apolo nchini
India.
WATOTO 2000 KATI YA 20,000 WAZALIWA WAKIWA NA TATIZO LA MOYO NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
March 13, 2018
Rating:

No comments