NAIBU WAZIRI NDITIE ASEMA KUWA SERIKALI INAENDELEZA KUTOA MAFUNZO YA TEHAMA.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia
uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa serikali
inaendeleza juhudi za kutoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano-TEHAMA kwa walimu wa shule za umma ili kabiliana na tatizo la ukosefu
wa ujuzi na upotevu wa fedha za serikali katika kuwalipa mafundi.
![]() |
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye. |
Naibu waziri Nditie ameyasema hayo mjini Dodoma wakati
akifungua mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa Shule za Sekondari za umma nchini
ambapo amesema kuwa ukosefu wa ujuzi wa TEHAMA umekuwa ukiisababishia serikali
hasara.
Akitoa maelezo ya Mafunzo hayo kwa niaba ya Mtendaji
Mkuu wa Mfuko wa Fursa sawa kwa wote MUKLAF, Katibu Mtendaji wa Mfuko huo Justina
Mashiba amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu katika ufundishaji
wa masomo ya TEHAMA.
Mafunzo hayo yametolewa kwa awamu ya pili baada ya
kukamilika kwa awamu ya kwanza ambayo imeshirikisha waliu mia mbili themanini
na sita.
NAIBU WAZIRI NDITIE ASEMA KUWA SERIKALI INAENDELEZA KUTOA MAFUNZO YA TEHAMA.
Reviewed by safina radio
on
March 13, 2018
Rating:

No comments