MAAFISA 5 WA POLISI NCHINI AFGHANISTAN WAMEUAWA

TAREHE 13-03-2018
Image result for PICHA YA MASHAMBULIZI NCHINI AFGHANISTANI


Afisa mmoja nchini Afghanistan amesema kiasi ya maafisa watano wa polisi nchini humo wameuawa baada ya waasi kushambulia eneo la ukaguzi katika jimbo la la magharibi la Farah.

Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo lakini kiongozi wa serikali kwenye jimbo hilo Fared Bakhtawer anawahusisha wanamgambo wa Taliban na shambulizi hilo.

Mwishoni mwa wiki wanamgambo wa Taliban waliwaua maafisa wa usalama 15 wa Afghanistan wakiwemo makamanda wajeshi saba na maafisa wa polisi wanane katika wilaya ya Bala Bluki.

 Haya yanajiri huku waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis akiwasili katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul katika ziara ambayo haikutangazwa.
MAAFISA 5 WA POLISI NCHINI AFGHANISTAN WAMEUAWA MAAFISA 5 WA POLISI NCHINI  AFGHANISTAN  WAMEUAWA Reviewed by safina radio on March 13, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.