WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY AMELIAMBIA BUNGE KUWA KUNA UWEZEKANO URUSI IMEHUSIKA KUMPA JASUSI SUMU

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amewaeleza wabunge nchini humo  kuwa kuna uwezekano Urusi imehusika na kumpa sumu jasusi wazamani Sergei Skripal pamoja na binti yake katika mji wa kusini wa Salisbury.


Image result for PICHA YA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY
                            Waziri Mkuu Theresa May

Waziri Mkuu Theresa May amesema iwapo ushahidi utathibitisha kuwa Urusi ilielekeza moja kwa moja tukio hilo basi serikali ya Uingereza itachukulia kuwa ni shambulizi lililofanywa kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria katika ardhi ya Uingereza.

Katibu Mkuu wa NATO - Jens Stoltenberg amesema tukio hilo linaibua wasiwasi mkubwa huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson akisema wana imani kubwa na uchunguzi unaofanywa na Uingereza pamoja na tathimini yake kuwa huenda Urusi ikawa inahusika na tukio hilo .

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY AMELIAMBIA BUNGE KUWA KUNA UWEZEKANO URUSI IMEHUSIKA KUMPA JASUSI SUMU WAZIRI MKUU WA UINGEREZA THERESA MAY AMELIAMBIA BUNGE KUWA KUNA UWEZEKANO URUSI IMEHUSIKA KUMPA JASUSI  SUMU Reviewed by safina radio on March 13, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.