NAIBU WAZIRI WA KILIMO DK. MARY MWANJELWA AMESEMA USHARIKA NI CHOMBO PEKEE KINACHOWEZA KUMKOMBOA MKULIMA
SONGWE.
Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwanjelwa amesema
usharika ndio chombo pekee kinachoweza kuleta ukombozi wa matokeo chanya kwa
mkulima.
![]() |
Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwanjelwa. |
Dk. Mwanjelwa ameyasema hayo mkoani Songwe wakati
akizungumza na wakulima wa Kahawa na wanunuzi wa zao hilo na amesisitiza kuwa kamwe
serikali haiwezi kuwapa mwanya walanguzi wa mazao ya wakulima ambao kwa muda
mrefu wamekuwa wakijinufaisha kupitia jasho la mkulima.
Aidha, amesema serikali ya awamu ya tano inawapenda na
kuwajali wakulima kwa wakati wote na imekuwa ikifanya mkakati wa kumwangali
mkulima ili aweze kunufaika kwa kiwango
fulani.
Amesema kuwa wakulima lazima wapende vyama vya
ushirika kwa kuwa ni vyombo vinavyoweza kuwasaidia
wakulima.
Hata hivyo, Baadhi ya wakulima wa Kahawa kutoka wilaya za Mbozi na Ileje wamepongeza hatua ya
serikali ya kufufua upya vyama vya ushirika jambo ambalo litakuwa na manufaa
kwa wakulima.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO DK. MARY MWANJELWA AMESEMA USHARIKA NI CHOMBO PEKEE KINACHOWEZA KUMKOMBOA MKULIMA
Reviewed by safina radio
on
March 06, 2018
Rating:

No comments