HUDUMA YA REDIO SAFINA JUMANNE HII INAKULETEA MAOMBI YA KUOMBEA MIPANGO WANAYOJIWEKEA ILI SHETANI ASIWANASE KATIKA MISINGI YA SIRI ILIYOBEBA ROHO YA MAANGAMIZI
ARUSHA.
Jamii imetakiwa kuombea mipango wanayojiwekea ili
shetani asiwanase kwenye misingi ya siri iliyobeba roho ya maangamizi ambayo
husubiri mtu afanikiwe au kupata cheo ndipo iweze kuachilia mabaya juu ya mtu
huyo.
![]() |
kuombea mipango. |
![]() |
misingi ya siri iliyobeba roho ya maangamizi kwa lengo la kushikilia maisha ya mtu baada ya kupata kitu kama vile elimu,cheo,ndoa au mafanikio yoyote. |
Kwa mujibu wa somo hilo misingi ya siri iliyobeba
roho ya maangamizi huachilia magonjwa baada ya mtu kupata mshahara,migogoro au
ndoa kuvunjika baada ya mtoto kuzaliwa,mwanafunzi kuchanganyikiwa au kujiua
baada ya kufaulu masomo,kupoteza maisha baada ya kupandishwa cheo pamoja na kuacha
waokovu baada ya kupata mafanikio.
![]() |
Kuchanganyikiwa bada ya mafanikio mbali mbali. |
Hata hivyo njia pekee inayoweza kuharibu misingi ya
siri iliyobeba roho ya maangamizi ni pamoja na mtu kumpokea Yesu kristo maisha
mwake, kuishi maisha ya toba siku zote, kudumu kwenye maombi ya muda
mrefu,pamoja na kuamini juu ya damu ya Yesu.
HUDUMA YA REDIO SAFINA JUMANNE HII INAKULETEA MAOMBI YA KUOMBEA MIPANGO WANAYOJIWEKEA ILI SHETANI ASIWANASE KATIKA MISINGI YA SIRI ILIYOBEBA ROHO YA MAANGAMIZI
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments