ZAIDI YA MADAKTARI 500 WA HOSPITALI YA KENYATTA, KENYA WAMESUSIA KAZI WAKITAKA KUREJESHWA KWA MWENZAO.
NAIROBI.
![]() |
Zaidi ya madaktari 500 katika hospitali kuu ya Kenyatta nchini Kenya wamesusia kazi. |
Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari nchini, Samuel
Oroko, amesema kumsimamisha kazi daktari huyo ilikuwa ni uamuzi ambao hauwezi
kutatatua shida zinazoikumba hospitali hiyo.
Muungano huo unataka mfumo mzima wa hospitali
kuchunguzwa, ikiwemo kuboresha mfumo wa kunakili data ya wagonjwa na pia
kuongezwa kwa idadi ya maeneo ya upasuaji.
Wiki iliyopita, Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya
taifa ya Kenyatta mjini Nairobi - Lily Koros - alipewa likizo ya lazima huku
Daktari na wahudumu katika hospitali hiyo wakisimamishwa kazi baada ya mgonjwa
kufanyiwa upasuaji wa kichwa kimakosa.
Mkasa huo ulitokana na mchanganyiko wa majina ya
wagonjwa wawili wote waliokuwa wana matatizo ya kichwa, na kosa halikujulikana
hadi mgonjwa mmoja alipopasuliwa kichwa ndani ya chumba cha upasuaji.
Hospitali ya Kenyatta ndio hospitali kubwa zaidi ya
umma nchini Kenya, na kusimamishwa kwa shughuli za matibabu huenda kukaathiri
shughuli katika hopsitali nyingine nchini humo.
Hata hivyo Takwimu
zinaonyesha kuwa hospitali ya Kenyatta huwapokea wagonjwa wasiopungua 3,000 kwa
siku.
ZAIDI YA MADAKTARI 500 WA HOSPITALI YA KENYATTA, KENYA WAMESUSIA KAZI WAKITAKA KUREJESHWA KWA MWENZAO.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments