TANZANIA YAENDELEA KUONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA NYANJA MBALI MBALI KIMATAIFA HUSUSANI KIUCHUMI.
DODOMA.
Imeelezwa kuwa,Tanzania imeendelea kuonyesha
mafanikio makubwa katika Nyanja mbali mbali kimataifa ikiwemo ya ukuaji wa
kiuchumi.
![]() |
Dk. Hassan Abas. |
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
Maelezo ambaye pia ni msemaji wa serikali Dk. Hassan Abas katika ripoti ya
mwezi February 2018 iliyotolewa na Shirika la Kimataifa inayoangazia masuala ya
Rushwa Transparency International mjini Dodoma.
Taarifa hiyo inaonesha kuwa Tanzania imepanda nafasi
13 duniani katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi huku ikishika nafasi ya
2 katika nchi za Afrika Mashariki ikitanguliwa na Rwanda.
Hali kadhalika, Dk. Abas amesema kuwa katika miradi
ya kuzalisha umeme wa kinyerezi 1 na 2 imefanikiwa kwa kuwa megawati 240 zinatarajiwa
kuzalishwa na Kinyerezi 2.
Hata hivyo, Dk. Abas amezungumzia mambo mengine
yanayohusiana na utekelezaji wa miradi mikubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya
Standard Gaurge kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na kasi kubwa ya ulipwaji wa
madeni ya watumishi na watoa huduma serikali ambapo zaidi ya bilioni 800 kati
ya trilioni 1 iliyotengwa na serikali imelipwa.
TANZANIA YAENDELEA KUONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA NYANJA MBALI MBALI KIMATAIFA HUSUSANI KIUCHUMI.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments