MWIGULU NCHEMBA AWATAKA MADEREVA BODABODA KUIFANYA SHUGHULI YAO KUWA YA HESHIMA, ARUSHA.
ARUSHA.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba
amewataka madereva wa bodaboda kuifanya shughuli yao kuwa shughuli ya heshima
kwani ni kazi ambayo ina mafanikio kwao na ni sehemu ya utoaji wa huduma kwa
jamii.
![]() |
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba. |
Mh. Nchemba ameyasema hayo wakati akizungumza na madereva wa bodaboda wa jiji la Arusha ambapo amesema kuwa kazi ya
kuendesha vyombo hivyo vya moto ni kazi ambayo imetoa fursa kwa vijana wengi
hivyo haina budi kuheshimiwa kama kazi nyingine .
Aidha,
amewataka madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha wanakuwa na kofia mbili ngumu ili kuweza kuepuka ajali zisizo za lazima na
upigwaji wa faini kutokana na makaosa ambayo mtu anaweza kukutwa nayo.
Naye, Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa
kutokana na kutokuwepo kwa fursa za mikopo katika benki nyingi, uongozi Mkoa
uliweza kuamua kutoa pikipiki 200 kwa Kata 25 huku kila kata ikipewa pikipiki 8
kwa lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi na kuweza kujiajiri wenyewe ambapo mpaka
sasa zaidi ya milioni 350
zimesharejeshwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa madereva wa
bodaboda jiji la Arusha Bw. Maulidi Makongoro katika risala yao amesema kuwa
umoja huo ulianzishwa Desemba 2016 kwa
lengo la kusimamia shughuli zote za waendesha bodaboda wa jiji la Arusha pamoja
na kushughulikia kero na ustawi wa maendeleo yao ambapo mpaka sasa umoja huo
una wanachama elfu tano.
MWIGULU NCHEMBA AWATAKA MADEREVA BODABODA KUIFANYA SHUGHULI YAO KUWA YA HESHIMA, ARUSHA.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments