UMOJA WA MATAIFA UMEIPONGEZA TANZANIA KUTOKANA NA HATUA ZA MAENDELEO INAZOCHUKUA.
KHATOOM.
Umoja wa Mataifa umeipongeza Tanzania chini ya Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli kutokana na
hatua za maendeleo inazochukua ambazo zimejengwa na misingi ya amani na utulivu
unaochangiwa na Jeshi la Ulinzi na Usalama La Tanzania –JWTZ.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi Maalumu wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya watoto na migogoro
ya kivita Virginia Gamba wakati wa ziara ya kukagua miradi ya watoto katika vijiji
vya Shangitobaya vinavyolindwa na wanajeshi wa Tanzania.
Aidha, amesema kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama Venance Mabeyo anapaswa kupongezwa kutokana na mafanikio ya vikosi vya wanajeshi walioshiriki na wanaoshiriki katika
operesheni mbali mbali zikiwemo za umoja wa Mataifa ni kielelezo cha kazi nzuri
ya jeshi hilo ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Hata hivyo, Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu aliyeambatana na Viongozi wa Sudan alipata nafasi ya
kuzungumza na wanajeshi wa Tanzania katika Kambi ya Shangitobaya kisha
kutembelea vituo vya watoto katika kijiji cha Shadayi nchini Sudan.
UMOJA WA MATAIFA UMEIPONGEZA TANZANIA KUTOKANA NA HATUA ZA MAENDELEO INAZOCHUKUA.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments