WASTANI WA MASHAMBULIZI YA 20 YAMEKUWA YAKIFANYWA NA NDEGE ZA JESHI LA URUSI.
WASHINGTON.
Marekani imesema
ndege za jeshi la Urusi zimekuwa zikifanya wastani wa mashambulizi 20 kila siku
dhidi ya ngome za waasi katika Ghouta ya Mashariki nchini Syria, kati ya tarehe
24 na 28 Februari.
![]() |
ndege za jeshi za Urusi katika mashambuzi Ghouta Mashariki. |
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema
mashambulizi dhidi ya waasi katika eneo hilo lililo karibu na mji mkuu-Damascus
yataendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Assad amesema
usitishaji mapigano wa masaa matano kila siku utaendelea, kutoa fursa kwa raia
wanaotaka kuondoka katika eneo hilo kufanya hivyo.
Rais huyo alikanusha shutuma kwamba jeshi la
serikali yake limetumia silaha za sumu, akiziita shutuma hizo kamusi ya uongo
ya nchi za Magharibi.
WASTANI WA MASHAMBULIZI YA 20 YAMEKUWA YAKIFANYWA NA NDEGE ZA JESHI LA URUSI.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments