SILVIO BERLUSCONI APATA NAFASI YA KUUNDA SERIKALI IJAYO KWA MATOKEO YASIYO RASMI KUPITIA MUUNGANO WA VYAMA ANAVYOVIONGOZA.
ROMA.
Matokeo yasio rasmi
yaliyochapishwa baada ya kufungwa kwa vituo vyote vya kupigia kura katika
uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Italia jana Jumapili, yanaupa nafasi kubwa
muungano unaoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Silvio Berlusconi
kuunda serikali ijayo.
![]() |
Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi. |
Katika Matokeo hayo
yanaonyesha kuwa vuguvugu hilo limejikusanyia asilimia 31.5 ya kura zote
zilizopigwa, wakati chama cha Demecratic kilichoko madarakani kikiambulia
asilimia 21.
Aidha vyama vinavyounda muungano unaoongozwa na
Berlusconi vimepata jumla ya asilimia 36; Forza Italia kimepata asilimia 16,
asilimia 16 nyingine zimekiendea chama cha Ligi ya Kaskazini, nacho chama cha
Ndugu wa Italia kina asilimia 4 ya kura
zote.
Hata hivyo, kwa
upande wa chama kimoja kimoja, Vuguvugu la Nyota Tano (M5S) limepata kura
nyingi zaidi.
SILVIO BERLUSCONI APATA NAFASI YA KUUNDA SERIKALI IJAYO KWA MATOKEO YASIYO RASMI KUPITIA MUUNGANO WA VYAMA ANAVYOVIONGOZA.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments