RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AMFUTA KAZI HENRY TUMUKUNDE NA KALE KAYIHURA KATIKA NYADHIFA ZAO.
KAMPALA.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amemfuta kazi Inspekta mkuu wa polisi,
Kale Kayihura na waziri wa Ulinzi, Henry Tumukunde.
![]() |
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. |
Generali Kayihura,
ambaye ni mkereketwa wa vita vilivyomsaidia rais Museveni kuingia madarakani
mwaka 1986, kwa wakati mmoja alikisiwa kuwa afisa mwenye mamlaka makubwa zaidi
katika jeshi la Uganda.
Lakini Generali
Kayihura amekuwa akikabiliwa na shinikizo kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu
wa usalama.
Zaidi ya wanawake 20
wameuawa katika visa vya mauaji ambavyo havijatatuliwa katika maeneo
yanayouzunguka mji mkuu wa Kampala, na katika miezi mitatu iliyopita raia
watatu wa kigeni pia wameuawa.
Naibu wake Okoth
Ochola anashikilia wadhifa huo.
Kwa mujibu wa ujumbe
alioandika rais Museveni katika mtandao wa Twitter, amesema kuwa, Kwa uwezo na
mamlaka aliliyopewa kikatiba, amemteua Jenerali Elly Tumwiine kama waziri wa
usalama, na bwana Okoth Ochola kama afisa mkuu wa polisi ambapo
Naibu wake atakuwa ni Brigedia Sabiiti Muzeei.
Hata hivyo Mnamo Mei
mwaka 2017 Rais Museveni alimteua upya Kayihura kama mkuu wa polisi kwa muhula
mwingine wa miaka mitatu,hadi mwaka 2020.
RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AMFUTA KAZI HENRY TUMUKUNDE NA KALE KAYIHURA KATIKA NYADHIFA ZAO.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments