MAHENGE AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA UMWAGILIAJI UNAOFADHILIWA NA WFP KUKAMILISHA MRADI HUO NDANI YA WIKI MBILI.
DODOMA.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Bilinith Mahenge ametoa
muda wa wiki mbili kwa mkandarasi wa mradi wa umwagiliaji maji unaofadhiliwa na
Shirika la Chakula Duniani WFP kukamilisha mradi huo uliotarajiwa kukamilika mwaka 2017 wilayani
Chamwino.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Bilinith Mahenge |
Maelekezo hayo yametolewa katika ziara yake ya
kutembelea na kukagua miradi ya kilimo inayotekelezwa wilayani Chamwino itakayogharimu
zaidi ya fedha shilingi milioni 18 ambapo vijiji vitatu vinatarajia kunufaika na
mradi huo.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kwa muda uliobaki mkandarasi
huyo hanabudi kupeleka mafundiwote katika eneo la mradi ili kuukmilisha kwa wakati
mbali na changamoto zilizopo.
Hata hivyo, Dk. Mahenge amemwagiza na kumtaka mkandarasi
huyo pamoja na mafundi wake wahakikishe wanatumia vizuri muda huo wa wiki mbili
.
\
MAHENGE AMTAKA MKANDARASI WA MRADI WA UMWAGILIAJI UNAOFADHILIWA NA WFP KUKAMILISHA MRADI HUO NDANI YA WIKI MBILI.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments