ZAIDI YA RAIA SABA WA ETHIOPIA WAMEKAMATWA MKOANI MWANZA.
MWANZA.
Zaidi ya wahamiaji haramu saba raia wa Ethiopia
wamekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed msangi amesema
kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunafuatia taarifa ya msamaria mwema aliyewatilia
shaka na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa watu kwenye kichaka katika
eneo la Nyenyeshishi wilayani Misungwi.
Aidha, amesema kuwa walikuwa na taarifa kutoka kwa
mtu huyo ambaye ni msamaria mwema iliyopelekea
kuagiza jeshi la polisi kufika maeneo hayo ya tukio ambapo lilifanikiwa kuwakamata watu hao.
Pia, Kamanda Msangi ameongeza kuwa wahamiaji
waliokamatwa ni raia tisa wa Ethiopia ambapo awali walikamatwa raia saba na
baadae raia wawili walikamatwa katika eneo jingine tofauti na hilo walipokuwa raia saba huku akidokeza kuwa wahamiaji hao hawajui lugha ya Kiswahili wala kingereza.
Hata hivyo, Kamanda Msangi ameongeza katika
mahojiano kati ya Polisi na Wahamiaji, wahamiaji hao walikuwa wakitamka neno Ethiopia
pekee kwa hiyo ni dhahiri kuwa waahamiaji hao ni raia wa Ethiopia.
Katika hatua nyingine Kamanda Msangi amewataka
wananchi kutanguliza uzalendo kwanza kuwafichua watu wanaoishi nchini kinyume
cha sheria pamoja na kutokuwa na vibali maalumu kwa vyombo vya dola ili kuwakamata
na kuwachunguza watu hao.
ZAIDI YA RAIA SABA WA ETHIOPIA WAMEKAMATWA MKOANI MWANZA.
Reviewed by safina radio
on
March 05, 2018
Rating:

No comments