MAOMBI MAALUM YAMEANDALIWA NA HUDUMA YA REDIO SAFINA ILI KILA MTU KUSIMAMISHA HATI YA KIFO MBELE ZA MUNGU KWA AJILI YA KUONYESHA WATU KUFIA MIGUU YA UKOO.
ARUSHA.
Jamii imeshauriwa kufahamu kuwa baada ya kusimamisha
hati inayoonesha kuwa wameshaifia miungu,Yesu Kristo atayakomesha mateso yote
yanayo wasumbua kwenye ndoa,uchumi,afya,elimu na changamoto zingine
zinazowadhibiti wasimtumikie Mungu kwa Roho na kweli.
![]() |
Yesu Kristo atayakomesha mateso yote. |
Redio safina kesho katika ukumbi wa maombi ulioko
Mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imeandaa
maombi ya maalum ya kila mtu kusimamisha hati ya kifo mbele za Mungu
inayoonesha kuwa wameifia miungu ya koo na familia lengo likiwa ni kurudishiwa
uzima wa milele wa kutokuharibika.
![]() |
kuuifia miungu ya koo na familia. |
Kwa mujibu wa somo hilo ziko roho,tabia na mienendo
ambayo inawatesa watu kama vile mimba kuharibika,kupatwa na magonjwa sugu,kuota
ndoto mbaya,migogoro ya ndoa,pamoja na uchumi kuyumba hali ambayo kila mmoja
hana budi kusimama na hati ya kifo mbele za Mungu inayoonesha kuwa walishayafia
hayo pamoja na Kristo hivyo shetani hapaswi tena kuwatesa.
![]() |
Migogoro ya ndoa. |
Pia somo hilo limebainisha kuwa zipo baadhi ya
dalili zinazoonesha kuwa mtu ameshikiliwa na roho ya miungu kama vile,kuzini
kwenye ndoto,kuacha shule bila sababu,kuchanganyikiwa au kufa,kusumbuliwa na
ndoto za nyoka,kulishwa vyakula usiku kwenye ndoto,kupitiliza muda muda wa wa
kuoa au kuolewa,siku za hedhi,kukandamizwa na roho ya umaskini,pamoja na
uchumba kuvunjika.
![]() |
Siku za hedhi. |
Hata hivyo kesho ni siku ya kuondoa roho zote za
miungu,magonjwa na matatizo yaliyokuwa yakiwatesa watu kutokana na kushikiliwa
na roho ya miungu.
MAOMBI MAALUM YAMEANDALIWA NA HUDUMA YA REDIO SAFINA ILI KILA MTU KUSIMAMISHA HATI YA KIFO MBELE ZA MUNGU KWA AJILI YA KUONYESHA WATU KUFIA MIGUU YA UKOO.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments