JUMLA YA FEDHA SHILINGI BILIONI 9.5 ZIMETOLEWA NA SERIKALI KWA UJENZI WA HOSPITALI WILAYANI MOMBA, SONGWE.
SONGWE.
Serikali imetenga jumla ya fedha shilingi bilioni
9.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe
hatua itakayowaondolea wananchi wa wilaya hiyo adha ya kusafiri umbali mrefu
kufuata huduma za afya.
Kwa Mujibu wa Mhandisi wa halmashauri ya Tunduma
Sospita Lukonja tayari serikali imekwisha kutoa bilioni 2.2 kwa wakala wa
majengo Tanzania TBA kwa ajili ya kuanza kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa
hospitali hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said
ameitaka TBA kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo katika muda uliopangwa na kwa
viwango vinavyokubalika.
JUMLA YA FEDHA SHILINGI BILIONI 9.5 ZIMETOLEWA NA SERIKALI KWA UJENZI WA HOSPITALI WILAYANI MOMBA, SONGWE.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments