ZAIDI YA FEDHA SHILINGI MILIONI 125 ZATOLEWA NA TASAF KWA UJENZI WA ZAHANATI YA MIDAWE.
ARUSHA.
Zaidi ya fedha shilingi milioni 125 zimetolewa na
TASAF kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi wa Zahanati ya Midawe kijiji cha
Bangata, Kata ya Bangata, katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC mkoani
Arusha.
![]() |
Fedha za mirdi ya TASSAF kwa wananchi. |
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Arusha DC Bw. Agrey Ngoka ambapo amewataka wananchi kusimamia kikamilifu mradi
huo kwa kuwa wananchi wasipofanya hivyo itasababisha serikali kurudi nyuma
katika utekelezaji wa mradi huo.
Aidha, Bw. Ngoka amesema kuwa kuna jumla ya miradi
kumi na moja katika awamu hiyo ya tatu ya mradi huo ambapo mradi wa mwisho utakaotekelezwa
ni mradi wa Tindoo wa kukarabati mfereji wa maji.
Hata hivyo Bw,Ngoka amewataka viongozi wa kata hiyo
ya Bangata pamoja na wananchi wote kwa ujumla kusimamia mradi huo kikamilifu
ili kuhakikisha kuwa hauzidi miezi mitatu kwa utekelezaji wake.
Kwa upande wake mratibu wa Tasaf Bi.Grace Makema
amewaomba wananchi wa kata ya Bangata pamoja na kijiji cha midawe kushirikiana
kwa pamoja katika kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo wamelenga
kukamilika kwa kipindi cha miezi mitatu.
Naye diwani wa kata hiyo Mh.Peter Mfere amewashukuru
Tasaf na kuahidi kuwa watashirikiana kwa nguvu zao zote kwa ajili ya kufanikishwa
kwa mradi huo wa zahanati ndani ya kata hiyo ya Bangata.
ZAIDI YA FEDHA SHILINGI MILIONI 125 ZATOLEWA NA TASAF KWA UJENZI WA ZAHANATI YA MIDAWE.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments