SEMAKAFU AWATAKA WAALIMU KANDA YA ZIWA NA KANDA YA MAGHARIBI KUPATIWA MAFUNZO YA MATUIZI YA TEHAMA.


MWANZA.

Kaimu katibu mkuu wa wizara ya elimu sayansi tekinolojia na mafunzo ya ufundi Bi Ave Maria Semakafu amewataka waalimu wa kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kupatiwa mafunzo ya matumizi ya habari na mawasiliano TEHAMA katika chuo cha ualimu Butimba jijini Mwanza.

Bi Ave Maria Semakafu 
Bi Semakafu ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakufunzi katika uzinduzi wa mafunzo hayo,ambapo amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha matumizi sahihi ya tekinolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA katika vyuo vya ualimu kote nchini licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali.

Amesema kuwa wao kama serikali hawataruhusu shule za sekondari za serikali na binafsi kufunguliwa bila kuwa na vyumba maalumu vya TEHAMA huku akiwataka wanafunzi hao kuwa na uzalendo ili kusaidia serikali kufikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa kati kwa njia ya viwanda.

SEMAKAFU AWATAKA WAALIMU KANDA YA ZIWA NA KANDA YA MAGHARIBI KUPATIWA MAFUNZO YA MATUIZI YA TEHAMA. SEMAKAFU AWATAKA WAALIMU KANDA YA ZIWA NA KANDA YA MAGHARIBI KUPATIWA MAFUNZO YA MATUIZI YA TEHAMA. Reviewed by safina radio on March 02, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.