WAKULIMA WA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFUA UTABIRI WAHALI YA HEWA UNAOTOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA.
ARUSHA.
Wakazi wa kanda ya Kaskazini hususani wakulima wametakiwa
kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa hapa
nchini ili waweze kukabiliana na majanga mbalimbali yanayosababishwa na
mbadiliko ya tabia nchi.
Wito huo umetolewa na mtaalamu wa mamlaka hiyo mkoa
wa Arusha Bw Justice Kijazi wakati akizungumza na Redio Safina kuhusu kuanza
kwa mvua za masika kwa mwaka huu wa 2018.
Bw Kijazi amesema kuwa ikiwa wakulima watafuatilia utabiri wa hali ya hewa
itawasaidia kuandaa mashamba yao mapema pamoja na kujua ni mazao gani
wanaopaswa kupanda na katika ukanda upi ili wasije kupata hasara na kukabiliana
na baa la njaa.
Amesema kuwa kwa mwaka huu wa 2018 katika mikoa ya
kanda ya Kaskazini ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara mvua za masika zitaanza
kunyesha wiki ya pili ya mwezi March na zinatarajiwa kukatika wiki ya tatu ya
mwezi Mei hivyo ni vyema wakafuatilia utabiri huo ili waanze kilimo chao kwa
wakati.
Hata hivyo ameongeza kuwa ili kuhakikisha mkulima
anafahamu umuhimu wa kufuatilia utabiri wa hali hewa wamekuwa wakitoa elimu kwa
njia mbalimbali ikiwemo Televisheni,Redio,na majarida mbalimbali.
WAKULIMA WA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFUA UTABIRI WAHALI YA HEWA UNAOTOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments