KIKOSI KAZI CHAUNDWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA PWANI ILI KUFUATILIA MADEREVA WANAOWASHAWISHI ASKARI KUPOKEA RUSHWA.
PWANI.
Jeshi la polisi mkoani Pwani limeanzisha kikosi kazi
maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva wanaowashawishi askari wao kupokea
rushwa pindi wanapokutwa na makosa mbalimbali ya usalama barabarani.
Hayo yameelezwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Pwani Jonathan Shana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani
humo,ambapo amesema kuwa jeshi hilo litawapandisha vyeo askari watakao wakamata
madereva wanaojaribu kuwashawishi wapokee rushwa.
Kamanda Shana amesema kuwa mkakati huo ni mojawapo
wa kupambana na ajali za barabarani mkoani Pwani.
Ameongeza kuwa kikosi kazi hicho kilichoundwa na
makachero kimeshaanza kazi na hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja kwa
madereva watakaokutwa na makosa hayo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo mkakati huo unalenga kuwafungia leseni na
pia kutangaza kwenye vyombo vya habari makampuni yote ya mabasi ambayo yatakuwa
yamekithiri kwa makosa ya mwendo kasi.
KIKOSI KAZI CHAUNDWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA PWANI ILI KUFUATILIA MADEREVA WANAOWASHAWISHI ASKARI KUPOKEA RUSHWA.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments