DOLA BILIONI 1.7 ZATARAJIWA KUCHANGISHWA NA WAFADHILI MBALIMBALI ILI KUFANIKISHA MISAADA YA KIBINADAMU.
KINSHASA.
Wafadhili mbalimbali wanatarajiwa kukutana mwezi ujao
kuchangisha Dola Bilioni 1.7 ili kufanikisha misaada ya kibinadamu kuwasaidia
mamilioni ya wakimbizi nchini DRC.
![]() |
Umoja wa Mataifa. |
Hatua hiyo imetangazwa na Umoja wa Mataifa, ambao umesema
unahitaji fedha hizo kufanikisha miradi yake katika taifa hilo ambalo
limekumbwa na ukosefu wa usalama eneo la mashariki hasa katika jimbo la Kasai.
Mkutano huo umepangwa kufanyika tarehe 13 mwezi ujao jijini
Geneva nchini Uswisi.
Wiki mbili zilizopita Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia
Wakimbizi (UNHCR) lilisema kuwa vurugu zinazoendelea kuongezeka katika mkoa wa
kusini mashariki mwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
zinachochea maafa ya kutisha ya kibinadamu.
Katika majuma mawili ya kwanza ya mwezi Februari, mashirika yanayoshirikiana
na UNHCR yaliorodhesha matukio mia nane, ikiwa ni pamoja na mauaji, utekaji
nyara na ubakaji huku vurugu nyingi zikitajwa kufanyika katika maeneo ambayo ni
vigumu kwa wafanyakazi wa kibinadamu kufika.
DOLA BILIONI 1.7 ZATARAJIWA KUCHANGISHWA NA WAFADHILI MBALIMBALI ILI KUFANIKISHA MISAADA YA KIBINADAMU.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments