JAE-IN APANGA KUTUMA MJUMBE MAALUMU KWENDA KOREA KASKAZINI.
SEOUL.
Rais wa Korea kusini
Moon Jae-in anapanga kutuma mjumbe maalum kwenda Korea kaskazini hivi karibuni
kutayarisha mazungumzo yatakayokuwa na maana zaidi kati ya mataifa hayo hasimu.
![]() |
Moon Jae-in Rais wa Korea kusini. |
Korea kusini ina matumaini
kuwa mazungumzo hayo hatimaye yatajumuisha majadiliano kuhusiana na Korea
kaskazini kuachana na mpango wake wa silaha za kinyuklia.
Ofisi ya rais wa Korea kusini imesema Moon
amewasilisha mpango huo kwa rais Donald Trump katika mazungumzo ya simu ya
dakika 30 jana Alhamisi ambapo ofisi hiyo haikusema Trump alichukuliaje hatua
hiyo.
Maafisa wa Korea
kaskazini waliotembelea Korea kusini kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya majira
ya baridi mjini Pyeongchang hivi karibuni wamesema kiongozi wao Kim Jong Un anataka
kufanya mkutano wa kilele na Moon na kwamba Korea kaskazini inapanga kuanzisha
mazungumzo na Marekani.
JAE-IN APANGA KUTUMA MJUMBE MAALUMU KWENDA KOREA KASKAZINI.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments