WAGOMBEA ITALIA WAPATA FURSA YAO YA MWISHO KUWAVUTIA WAPIGA KURA HII LEO.
ROME.
Kampeni za uchaguzi
nchini Italia uliopangwa kufanyika tarehe 4 Jumapili zinamalizika leo.
![]() |
Silvio Berlusconi |
Silvio Berlusconi
pamoja na wagombea wengine katika uchaguzi huo ambao hautabiriki wanapata fursa
yao ya mwisho kuwavutia wapiga kura hii leo.
Berlusconi anaongoza
muungano wa vyama vya mrengo wa kulia ambao unatarajia kupata ushindi dhidi ya
vuguvugu la kupinga utawala wa Five Star (M5S) pamoja na chama tawala cha siasa
za wastani za mrengo wa kushoto cha Democraric DP, lakini muungano wa vyama
hivyo hauna hakika ya kupata wingi wa viti katika bunge.
Berlusconi mwenye
umri wa miaka 81 ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Italia amekuwa akifanya
mahojiano ya televisheni na redio tu na kujiweka mbali na heka heka za kampeni
za kwenda huku na huko.
WAGOMBEA ITALIA WAPATA FURSA YAO YA MWISHO KUWAVUTIA WAPIGA KURA HII LEO.
Reviewed by safina radio
on
March 02, 2018
Rating:

No comments