MAJALIWA AWAAGIZA VIONGOZI WA WILAYA YA TANDAHIMBA KUHAKIKISHA KUWA WANADHIBITI ONGEZEKO LA MIMBA KWA WANAFUNZI WA KIKE.
MTWARA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Majaliwa Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa wilaya ya Tandahimba Mkoani
Mtwara kuhakikisha kuwa wanadhibiti ongezeko la mimba kwa wanafunzi.
![]() |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa |
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati akizungumza na
watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba huku akiongeza
kuwa lazima viongozi hao wasimamie nidhamu kwa kuwasimamia watoto wa kike ili
waendelee na masomo yao shuleni pamoja na kutaka kukamatwa na kuchukuliwa kwa
hatua za kisheri kwa wote wanaohusika na
kusababisha ujauzito kwa wanafunzi.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa mwaka 2016 mimba za
utotoni ziliongezeka kutoka idadi ya mimba kumi hadi mimba ishirini ambapo ni idadi kubwa hivyo
jamii inapoteza wanafunzi wengi wa kike japo kuwa kuna wawakilishi na wasimamizi
wa wananchi ambao walitakiwa kuonesha utaifa kwanza.
Hali kadhalika, Mh. Majaliwa amebainisha kuwa kwa
2017 mimba ziliongezeka kutoka idadi ya mimba ishirini hadi kufikia idadi ya
mimba hamsini na saba jambo linalopelekea kupoteza idadi kubwa ya wanafunzi wa
kike.
Hata hivyo, Mh. Majaliwa ameonesha hali ya kukerwa
na hatua zinazofanywa na viongozi wa wilaya hiyo hususani watumishi hasa Afisa
elimu, Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama
wakiwa hawachukui hatua zozote kuhusiana na suala hilo.
Katika Hatua Nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ametoa
wito kwa watumishi wa umma kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa
uadilifu na kwa kufuata sheria.
MAJALIWA AWAAGIZA VIONGOZI WA WILAYA YA TANDAHIMBA KUHAKIKISHA KUWA WANADHIBITI ONGEZEKO LA MIMBA KWA WANAFUNZI WA KIKE.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments