HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU INATARAJIA KUPITIA BAJETI YAKE KUTOKANA AGIZO LA WAZIRI JAFFO.
ARUSHA
Kufuatia agizo lililotolewa na waziri wa nchi ofisi
ya Rais Tawala za mikoa,na serikali za mitaa TAMISEMI Mh suleman Jaffo kwa
wenyeviti wa halmashauri nchi nzima kupitia bageti zao upya, halmashauri ya Meru
inatarajia kupitia bageti yake kwa kutoa vipaumbele katika elimu na sekta ya
Afya.
![]() |
Mh suleman Jaffo |
Akizungumza na Safina Redio ofisini kwake wilayani Arumeru
mwenyekiti wa halmashauri ya Meru Wille Njau amesema kuwa kutokana na agizo
hilo la Mh waziri halmashauri yake itachagua na kutekeleza miradi itakayoleta
manufaa kwa wananchi.
Aidha mwenyekiti huyo amesema moja kati ya mambo
watakayotoa kipaumbele wakati wa kupitia bageti hiyo ni pamoja na mradi wa
shule za sekondari ikiwemo shule ya sekondari
Uwiro na Nansio pamoja na vituo vya afya na zahanati ambazo
hazijakamilika.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amewataka wakulima kuandaa mashamba mapema ili
kupanda mazao yao kwa wakati na hiyo itawasaidia kuepukana na janga la njaa.
HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU INATARAJIA KUPITIA BAJETI YAKE KUTOKANA AGIZO LA WAZIRI JAFFO.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments