ZAIDI YA WANAFUNZI LAKI 6 WATAKAA NYUMBANI KUTOKANA NA MGOMO UTAKAOFANYWA NA WAHADHIRI WA VYUO VIKUU NCHNI KENYA.
NAIROBI.
Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya umma nchini Kenya, wameanza
mgomo kwa madai ya kwamba serikali imeshindwa kutekeleza mkataba wa kuwaongezea
mshahara kama ilivyokubaliwa mwaka uliopita.
Chuo Kikuu cha Sheria cha Nairobi Kenya. |
Constatine Wasonga, Katibu Mkuu wa muungano wa wahadhiri
nchini humo UASU, amesema serikali imeshindwa kuheshimu makubaliano waliofikia
na imewadharau,ambapo mgomo huo utasababisha zaidi ya wananfunzi Laki 6 kukaa
nyumbani.
Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni Kenya ilikabiliwa
na migomo ya hapa na pale, hasa katika sekta ya afya na elimu na migomo hiyo
mara nyingi imekua ikisababishwa na suala la nyongeza ya mshahara kwa
wafanyakazi katika sekta hizo.
ZAIDI YA WANAFUNZI LAKI 6 WATAKAA NYUMBANI KUTOKANA NA MGOMO UTAKAOFANYWA NA WAHADHIRI WA VYUO VIKUU NCHNI KENYA.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:
No comments