MAREKANI, MAPIGANO YANAYOENDELEA KATIKA NGOME YA UPINZANI YA GHOUTA MASHARIKI NI ISHARA TOSHA KUWA AZIMIO LA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEPUZWA.

WASHINGTON.
Marekani imeishtumu Urusi na serikali ya Syria kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano Mashariki mwa Ghouta, licha ya kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Raia wanaendelea kuyatoroka makazi yao kufuatia mashambulizi mashariki mwa Ghouta.
Marekani inasema mapigano yanayoendelea kushuhudiwa katika ngome hiyo ya upinzani, ni ishara tosha kuwa azimio hilo lililopitishwa Jumamosi iliyopita,halijaheshimiwa.
Katika mkataba ilikubaliwa kuwa, vita vingesitishwa kwa muda wa siku 30 katika ngome hiyo ya upinzani ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa wa vita vinavyoendelea.
Urusi ambayo inasaidia Syria, imeamua kuwa usitishwaji wa mapigano utadumu kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, ili kuwaruhusu raia wa kawaida kuondoka katika ngome hiyo ya upinzani.
Kauli hiyo ya Marekani imekuja wakati huu wakati mashirika ya kutetea haki za binadamu yakisema kuwa raia wa kawaida wapatao mia sita waliuawa mwezi Februari katika ngome ya upinzani ya Ghouta.

MAREKANI, MAPIGANO YANAYOENDELEA KATIKA NGOME YA UPINZANI YA GHOUTA MASHARIKI NI ISHARA TOSHA KUWA AZIMIO LA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEPUZWA. MAREKANI, MAPIGANO YANAYOENDELEA KATIKA NGOME YA UPINZANI YA GHOUTA MASHARIKI NI ISHARA TOSHA KUWA AZIMIO LA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA  LIMEPUZWA. Reviewed by safina radio on March 01, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.