HOMA YA LISSA YAUA MAKUMI YA WATU NCHINI NIGERIA.
ABUJA.
Wizara ya Afya ya Nigeria imetangaza kuwa makumi ya watu
wamefariki dunia nchini humo kutokana na maambukizi ya homa ya Lassa.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Nigeria imesema kuwa,
kesi 193 za maambukizi ya homa ya Lassa zimeshuhudiwa katika majimbo 17 ya nchi
hiyo kwenye kipindi cha miezi miwili iliyopita na kwamba watu 43 wamefariki
dunia kutokana na homa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia
kutokana na homa hiyo ni sawa na asilimia 24 ya kesi zote zilizothibitisha uwepo wa ugonjwa huo kote nchini
Nigeria.
Wakati huo huo Shirika la Afya duniani WHO
limesema kuwa idadi mpya ya waathirika wa homa ya Lassa ambayo imetolewa
na kituo cha kudhibiti magonjwa cha Nigeria-NCDC- inaonesha kuwa kati ya
Januari Mosi na Februari 25 mwaka 2018, visa elfu moja na themanini vya homa ya
Lassa viliripotiwa na kwamba watu 90 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa
huo.
Wizara ya Afya ya Nigeria imesema kwa kawaida ugonjwa wa homa wa
Lassa husambaa katika kipindi cha ukame lakini sasa unashuhudiwa katika vipindi
na misimu yote ya mwaka.
Ugonjwa wa homa ya Lassa ulishuhudiwa kwa mara ya kwana nchini
Nigeria mwaka 1969 katika mji wa Lasa na kwa sababu hiyo ulipewa jina la mji
huo ambapo wataalam wanasema kuwa Ugonjwa huo unashabihiana sana na ule wa
Ebola.
HOMA YA LISSA YAUA MAKUMI YA WATU NCHINI NIGERIA.
Reviewed by safina radio
on
March 01, 2018
Rating:

No comments