JESHI LA RWANDA LASEMA WANAJESHI WATATU WA DRC WAMEUAWA.


KIGALI.



Jeshi la Rwanda limesema kuwa wanajeshi watatu wa Jamhuri ya Democrasia ya kongo DRC wameuawa kwenye mapambano baada ya kushambulia kituo cha jeshi la Rwanda kwenye wilaya ya musanze kaskazini mashariki mwa Rwanda.

Hatua hii imekuja siku chache baada ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo kushutumu kuwa wanajeshi wa Rwanda wamevamia ardhi yake 
siku ya jumatano.



Msemaji wa jeshi la demokrasia ya kongo amesema mapigano makali yalizuka kati ya jeshi la DRC na wapiganaji wa jeshi la Rwanda katika eneo la mlima Nikone kwenye jimbo la kivu kaskazini na kuripoti tukio hilo kwa kundi la nchi za maziwa makuu.

Kwa upande wake Msemaji wa divisheni ya pili ya jeshi la Rwanda Bw Eugen Nkubito amesema kuwa majeshi ya DRC yameshambulia vikosi vyake katika kijiji cha iterambere jumanne asubuhi na kuwaua wapiganaji watatu na kuwafukuza wengine.


JESHI LA RWANDA LASEMA WANAJESHI WATATU WA DRC WAMEUAWA. JESHI LA RWANDA LASEMA WANAJESHI  WATATU WA DRC WAMEUAWA. Reviewed by safina radio on February 16, 2018 Rating: 5

No comments