Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk. John Pombe Maguli hii leo amehudhuria Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Kampala nchini Uganda.
KAMPALA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk. John
Pombe Maguli hii leo amehudhuria Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki mjini Kampala nchini Uganda.
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na tafiti
zilizofanywa na Jopo la Nchi za Afrika linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Afrika
Kusini Tabo Mbeki inaeleza kuwa nchi za Afrika zinapoteza wastani wa dola
bilioni 150 kila mwaka kutokana na utoroshaji wa rasilimali nje ya nchi.
Amesema kuwa Tanzania kwa sasa imeanza kukusanya mapato ya ndani kutoka vyanzo
mbalimbali vya mapato yanayofanikisha ujenzi wa treni ya kisasa itakayogharimu kiasi
cha dola za marekeani bilioni 3.5.
Hata hivyo, Mkutano huo wa wakuu wa nchi wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki umelenga kurejelea
mikutano ya nyuma iliyofanyika mwaka 2004, 2012, na 2014 na kutoa msaada wa
msukumo wa kisiasa katika kuunganisha mchakato wa agenda katika ukanda wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kutekeleza mipango ya kimaendeleo.
Mkutano huo
pia umehudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Jumaiya ya Afrika Mashariki ambao ni Rais
Kaguta Museven wa Uganda, Uhuru Kenyata wa Kenya, na Salva Kir wa Sudani
Kusini, huku wakuu wa nchi za Rwanda na Burundi wakiwa wametuma wawakilishi wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk. John Pombe Maguli hii leo amehudhuria Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Kampala nchini Uganda.
Reviewed by safina radio
on
February 22, 2018
Rating:

No comments