Mahakama nchini Iraq imewahukumu adhabu ya kifo wanawake 16 wa Kituruki waliokutwa na hatia ya kuwa Wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislam-IS.
BAGDAD.
Mahakama nchini Iraq imewahukumu adhabu ya kifo
wanawake 16 wa Kituruki waliokutwa na hatia ya kuwa Wanachama wa kundi la
kigaidi linalojiita Dola la Kiislam-IS.
![]() |
Baadhi ya wanawake kutoka nchini Uturuki walishtakiwa nchini Iraq |
Baadhi ya wanawake
hao wenye umri wa miaka 20 hadi 50, waliingia Iraq na watoto wadogo ambapo Wanawake hao
waliiambia mahakama kwamba waliingia nchini Iraq kinyume na sheria kuwafuata
waume zao ambao ni wanamgambo wa kundi la IS.
Iraq imeshawakamata
wanawake 560 na watoto 600 wanaodaiwa kuwa na uhusiano na kundi la IS, na
imeharakisha kuwafungulia mashtaka.
Shirika la Kimataifa
la Kutetea Haki za Binaadamu, Human Rights Watch limesema hukumu hiyo si ya haki,
huku baadhi ya wanaharakati wakihoji kwamba wengi wao walidanganywa au
kulazimishwa kujiunga na kundi hilo la kigaidi.
Mahakama nchini Iraq imewahukumu adhabu ya kifo wanawake 16 wa Kituruki waliokutwa na hatia ya kuwa Wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislam-IS.
Reviewed by safina radio
on
February 26, 2018
Rating:

No comments