IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI YA ANGA NCHINI SYRIA YAFIKIA 250

TAREHE 21-02-2018


Idadi ya watu waliokufa katika mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya serikali  huko Ghouta mashariki imefikia 250 ambapo kati ya idadi hiyo 50 wakiwa ni watoto.

Umoja wa mataifa nchini Syria umesema una mashaka makubwa juu maisha ya mamia ya raia ambao bado wapo katika eneo linalolengwa na mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali ya Syria katika eneo la Ghouta mashariki.

Mashambulizi hayo yaliyoanza siku ya jumapili bado yanaendelea na kusababisha vifo na majeruhi wengi wakiwemo watoto.

Umoja wa mataifa umeelezea mashaka yake juu ya kutokea Allepo nyingine,ambapo ukombozi wa mji huo mwaka 2016 pia ulisababisha vifo vya mamia ya raia kufuatia mashambulizi ya vikosi vya serikali.

IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI YA ANGA NCHINI SYRIA YAFIKIA 250 IDADI YA WATU WALIOKUFA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI YA ANGA NCHINI SYRIA YAFIKIA 250 Reviewed by safina radio on February 21, 2018 Rating: 5

No comments