ZUMA APEWA SIKU MBILI NA CHAMA CHAKE KUACHIA NGAZI

TAREHE 13-02-2018




Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC kimemtaka Rais Jacob Zuma kuachia madaraka kama kiongozi wa taifa hilo.

Ripoti kutoka ndani ya kamati kuu ya chama hicho zimesema kwamba Zuma amepewa siku mbili za kujiuzulu. 

Hatua hii inatokea baada ya kikao kilichodumu kwa muda wa saa 13 na kuhusisha viongozi wa juu wa chama.

Rais Jacob Zuma ametakiwa kuachia madaraka na chama chake mwenyewe cha ANC mapema hii leo, kufuatia wiki moja ya minong'ono kuhusiana na hatma ya uongozi wake.

Iwapo atagoma kujiuzulu anaweza kukabiliwa na kura ya bunge ya kutokuwa na imani naye, wakati ambapo tayari tarehe ya kura hiyo ilikwishapangwa kuwa ni Februari 22.


ZUMA APEWA SIKU MBILI NA CHAMA CHAKE KUACHIA NGAZI ZUMA APEWA SIKU MBILI  NA CHAMA CHAKE  KUACHIA NGAZI Reviewed by safina radio on February 13, 2018 Rating: 5

No comments