ZIJLSTRA ATANGAZA KUJIUZULU WADHIFA WAKE HAPO JANA KUTOKANA NA KUTOKUHUDHURIA MKUTANO WA RAIS.


AMSTERDAM.

Taarifa ya Habari saa 01:00 mchana, 14 February, 2018.
Halbe Zijlstra, Waziri wa Mambo ya kigeni wa Uholanzi.


Waziri wa Mambo ya kigeni wa Uholanzi, Halbe Zijlstra ametangaza kujiuzulu wadhifa wake hapo jana kufuatia ufichuzi kwamba alidangaya kuhusu kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na rais wa Urusi.

Waziri huyo amekabiliwa na ongezeko la wito wa kumtaka kuachia madaraka kutoka upande wa upinzani baada ya kukiri siku ya Jumatatu kwamba alisema uongo kuhusu kuwa mgeni katika mkutano ulioandaliwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin muongo mmoja uliopita.

Waziri mdogo wa wizara hiyo nchini Uholanzi Sigrid Kaag, aliyeongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioharibu silaha za sumu nchini Syria mwaka 2013, atachukua majukumu ya waziri Zijlstra hadi hapo atakapotajwa waziri mwingine atakayeongoza wizara hiyo.

ZIJLSTRA ATANGAZA KUJIUZULU WADHIFA WAKE HAPO JANA KUTOKANA NA KUTOKUHUDHURIA MKUTANO WA RAIS. ZIJLSTRA ATANGAZA KUJIUZULU WADHIFA WAKE HAPO JANA KUTOKANA NA KUTOKUHUDHURIA MKUTANO WA RAIS. Reviewed by safina radio on February 14, 2018 Rating: 5

No comments