KAMKET APENDEKEZA MSWADA BUNGENI UNALENGA KUBADILISHA MFUMO WA KATIBA.


NAIROBI.
Mbunge wa chama cha KANU nchini Kenya Kassait Kamket, amependekeza mswada bungeni unaolenga kubadilisha mfumo wa uongozi nchini humo kwa kuibadilisha Katiba.
Mbunge wa chama cha KANU nchini Kenya Kassait Kamket.
Habari zinasema kuwa iwapo Mswada huo utakubaliwa na wabunge, ina maana kuwa Katiba mpya ya Kenya iliyopatikana mwaka 2010, itafanyiwa mabadiliko makubwa.
Mbunge huyo anapendekeza kuundwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu atakayekuwa na madaraka makubwa lakini pia kuwepo kwa rais ambaye atakuwa ishara ya umoja wa kitaifa.
Iwapo marekebisho hayo yatafanyika, bunge la pamoja, lile la kitaifa na Senate litamchagua rais ambaye atakuwa na jukumu la kumteua Waziri Mkuu kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi bungeni.
Waziri Mkuu atahudumu kwa muda wa miaka mitano kabla ya Uchaguzi mwingine kufanyika, huku rais ambaye ni lazima awe na zaidi ya miaka 50, akihudumu kwa muhula mmoja wa miaka saba.
Wanasiasa wa upinzani na viongozi wa dini wamekuwa wakisema mfumo huu ndio utakaosaidia kumaliza mvutano wa kihistoria wa kisiasa hasa kuhusu wadhifa wa urais.
KAMKET
KAMKET APENDEKEZA MSWADA BUNGENI UNALENGA KUBADILISHA MFUMO WA KATIBA. KAMKET APENDEKEZA MSWADA BUNGENI UNALENGA KUBADILISHA MFUMO  WA KATIBA. Reviewed by safina radio on February 28, 2018 Rating: 5

No comments