SERIKALI IMESEMA TATIZO LA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI LIMEKUWA KUBWA.
TAREHE O9 FEB 2018
Serikali imesema tatizo la matumizi ya dawa za
kulevya hapa nchini limekuwa kubwa na kuathiri vijana wengi huku bangi ikiwa
dawa inayotumika zaidi na mmea huo ukiwa unastaishwa kwa wingio katika mikoa ya
Mara, Mbeya, Njombe, Morogoro, Arusha, Tanga, Kagera, na Iringa.
Hayo yamebainishwa mjini Dodoma na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Mh. Jenista Muhagama wakati akizungumzia
athari za dawa za kulevya nchini na uthibiti wake ambapo
amesema tafiti zilizofanyika nchini mwaka 2014 zinaonesha watu kati ya laki
mbili na elfu hamsini hadi laki tano wanatumia dawa za kulevya aina ya heroin.
Aidha, Waziri Muhagama amebainisha kuwa katika tafiti
hiyo kati ya watu hao laki mbili na elfu hamsini hadi laki tano, watu wapatao
elfu thelethini wanatumia dawa hiyo kwa njia ya kujidunga.
Hata hivyo, Kamishna wa Tiba na Kinga wa Mamlaka ya kudhibiti
na Kupambana Madawa ya Kulevya Peter Mpisi amesema kuwa katika kipindi kifupi mamlaka
hiyo imekuwa ikipokea watu wengi wanaohitaji msaada kwa ajili ya vijana
waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya kutokana na kudhibitiwa kwa matumizi
yake.
Hata hivyo serikali
itaendelea na ujenzi wa hospitali hiyo kulingana na upatikanaji wa fedha ili
wananchi waweze kupata huduma.
SERIKALI IMESEMA TATIZO LA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI LIMEKUWA KUBWA.
Reviewed by safina radio
on
February 09, 2018
Rating:
No comments