KOREA KASKAZINI IMEFUTA MKUTANO WA SIRI ULIOTARAJIWA KUFANYIKA KATI YAKE NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI


PYONGYANG.

Korea Kaskazini imefuta mkutano wa siri uliotarajiwa kufanyika kati yake na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence wakati wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ikiendelea nchini Korea Kusini.

Nick Ayers 
Mkuu wa utumishi wa makamu wa rais Nchini Marekani, Nick Ayers ameilaumu serikali ya Korea Kaskazini akisema inasimamia matakwa ya kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un kuyafunika mauaji yanayofanywa na utawala wake, kwa kupiga picha nzuri kwenye michezo hiyo na ndio maana wamefuta mkutano huo ama hawakuwa wakweli kuhusu kufanya mkutano huo.

Pence aliongoza ujumbe wa Marekani katika michezo hiyo ya Olimpiki.
Pia Bw Pence Alisafiri na baba mzazi wa Otto Warmbier ambaye mwanaye alifariki muda mfupi baada ya kuachiwa huru kutoka kizuizini nchini Korea Kaskazini akiwa kwenye koma (yaani hali mbaya mahututi) ili kuikumbusha dunia kuhusu mateso yanayofanywa nchini Korea Kaskazini.

KOREA KASKAZINI IMEFUTA MKUTANO WA SIRI ULIOTARAJIWA KUFANYIKA KATI YAKE NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KOREA KASKAZINI IMEFUTA MKUTANO WA SIRI ULIOTARAJIWA KUFANYIKA KATI YAKE NA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI Reviewed by safina radio on February 21, 2018 Rating: 5

No comments