Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameitisha uchaguzi mkuu wa mapema utakao ambatana na kura ya rais mnamo April 22 mwaka huu. Maduro amesema kuwa uchaguzi mkuu unapaswa kuhusisha bunge, halmashauri na mamlaka za manispaa ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo mageuzi kamili.
CARACAS.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameitisha uchaguzi
mkuu wa mapema utakao ambatana na kura ya rais mnamo April 22 mwaka huu.
Maduro amesema kuwa uchaguzi mkuu unapaswa kuhusisha
bunge, halmashauri na mamlaka za manispaa ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo mageuzi
kamili.
Rais huyo
amesema mabunge yote yenye nguvu yataamua ikiwa kufanyike uchaguzi wa bunge
miaka miwili kabla ya ilivyopangwa.
Ikiwa
Venezuela itaendelea na uchaguzi mkuu, inaweza kuathiri udhibiti wa upinzani
bungeni baada ya muungano mkuu wa upinzani kutangaza kususia uchaguzi wa rais
mapema siku ya Jumatano.
Muungano huo unasema hauwezi kushiriki katika
uchaguzi huo kama hakuna hakikisho kutoka kwa serikali kwamba uchaguzi huo
utakuwa huru na wa haki.
Muda mfupi
baada ya tangazo hilo la upinzani, Maduro amesema uchaguzi utafanyika kama
ulivyopangwa licha ya mazingira hayo.
Serikali ya Venezuela imejitahidi kukabiliana na
mgogoro wa kiuchumi baada ya bei ya mafuta kushuka mwaka 2014.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameitisha uchaguzi mkuu wa mapema utakao ambatana na kura ya rais mnamo April 22 mwaka huu. Maduro amesema kuwa uchaguzi mkuu unapaswa kuhusisha bunge, halmashauri na mamlaka za manispaa ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo mageuzi kamili.
Reviewed by safina radio
on
February 22, 2018
Rating:

No comments