MAJALIWA AAGIZA KUKAMATWA KWA DAKTARI WA KITUO CHA AFYA CHA MAHUTA MKOANI MTWARA KUTOKANA NA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU WIZI WA DAWA.



MTWARA.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa kwa Daktari wa kituo cha afya cha Mahuta mkoani Mtwara kufuatia malalamiko ya wananchi yanayodai kuwa daktari huyo amehusika na wizi wa dawa unaosababisha wananchi kukosa huduma hiyo.

Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh Majaliwa ametoa maagizo hayo katika mji mdogo wa Mahuta baada ya wananchi wa eneo hilo kusimamisha msafara wake na kuomba kutatuliwa kero hiyo.

Amesema kuwa serikali imeshapiga marufuku dawa zinazopelekwa kwenye Zahanati na vituo vya afya kutumika kinyume cha sheria,hivyo daktari huyo anapaswa kukamatwa na kurudisha dawa hizo na kisha kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuboresha huduma za afya kwa kutoa fedha kila mwaka kiasi cha shilingi milioni 120 katika kila Halmashauri,ambapo ametoa wito kwa Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha kuwa kila zahanati na kituo cha afya kinakuwa na dawa za kutosha.

MAJALIWA AAGIZA KUKAMATWA KWA DAKTARI WA KITUO CHA AFYA CHA MAHUTA MKOANI MTWARA KUTOKANA NA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU WIZI WA DAWA. MAJALIWA AAGIZA KUKAMATWA KWA DAKTARI WA KITUO CHA AFYA CHA MAHUTA MKOANI MTWARA KUTOKANA NA MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU WIZI WA DAWA. Reviewed by safina radio on February 28, 2018 Rating: 5

No comments