MAGUFULI ATOA MSAADA WA FEDHA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 18 KWA HOSPITALI YA MANYAMA NYAMA.


MARA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametoa msaada wa vitanda ishirini na tano, magodoro ishirini na mashuka hamsini vyote vikiwa na thamani ya fedha zaidi ya shilingi milioni 18 ili kuimarisha upatikanaji wa tiba katika hospitali ya wilaya ya Bunda ya Manyama nyama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agnes Methew ametoa wito kwa wataalamu wa afya wa hospitali hiyo kutimiza wajibu wao wa kuhudumia wagonjwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bunda Janeth Mayanja pamoja na Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Nicodemas Masosota wamesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kutoa mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo.

Hospitali ya wilaya ya Bunda ya Manyamanyama kwa kipindi kirefu imekuwa ikikimbiwa na wagonjwa kutokana na ukosefu wa vifaa tiba pamoja na wataalamu wa afya ambapo wagonjwa wengi wanalazimika kusaka tiba katika hospitali ya Bunda BBH.

MAGUFULI ATOA MSAADA WA FEDHA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 18 KWA HOSPITALI YA MANYAMA NYAMA. MAGUFULI ATOA MSAADA WA FEDHA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 18 KWA HOSPITALI YA MANYAMA NYAMA. Reviewed by safina radio on March 01, 2018 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.