REX TILLERSON AWATAKA WASHIRIKA WA MAREKANI KUENDELEA NA VITA DHIDI IS
WASHINGTON.
Taarifa ya Habari 08:00 Usiku,13 February, 2018.
![]() |
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Rex Tillerson akizungumza jambo na washirika wa Marekani. |
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Marekani, Rex Tillerson, amewataka washirika wa Marekani kuendeleza vita dhidi
ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS, akisema kumalizika kwa operesheni
kabambe dhidi ya kundi hilo hakumaanishi kuwa limeshindwa kabisa.
Tillerson ameyasema hayo leo katika
mkutano wa ngazi ya mawaziri unaoendelea katika mji mkuu wa Kuwait, kuhusu vita
dhidi ya IS na ukarabati wa Iraq.
Waziri Tillerson amesema IS bado ni
kitisho cha usalama kwa kanda, wa baadhi ya mataifa washirika, na kwa baadhi ya
sehemu nyingine duniani.
Desemba mwaka uliopita, Iraq ilitangaza
kulishinda kundi hilo la kijihadi, lakini bado linashikilia maeneo nchini
Syria.
Mapambano dhidi ya kundi hilo yamepata
changamoto kutokana na operesheni zinazoungwa mkono na Uturuki, kaskazini mwa
Syria, dhidi ya makundi ya Wakurdi ambayo ni washirika wa Marekani.
REX TILLERSON AWATAKA WASHIRIKA WA MAREKANI KUENDELEA NA VITA DHIDI IS
Reviewed by safina radio
on
February 13, 2018
Rating:

No comments