MAGAIDI WASIOPUNGUA 12 WAMEUAWA NA JESHI LA MISRI KASKAZINI MWA RASI YA SINAI.
CAIRO.
12 February, 2018.
![]() |
Jeshi la Misri likiwa katika operesheni kubwa dhidi ya ugaidi kaskazini mwa Rasi ya Sinai. |
Jeshi la Misri
limesema kuwa limeua magaidi wasiopungua 12 na kuwatia mbaroni wengine wapatao
100 katika opereseheni kubwa iliyoanzishwa na jeshi hilo kaskazini mwa Rasi ya
Sinai.
Taarifa
hiyo ya jeshi la Misri imetolewa leo Jumatatu, siku moja baada ya jeshi hilo
kutangaza jana kwamba limeua magaidi 16 katika opesheni kama hiyo.
Taarifa
ya jeshi la Misri imeongeza kuwa ndege za kivita za nchi hiyo zimeshambulia maeneo
60 yakiwemo magari, maghala ya silaha na vituo vya mawasiliano vya magaidi.
Pia
taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana imesema kuwa, washukiwa wengine 30
wametiwa mbaroni katika operesheni hiyo ya kijeshi iliyoanza katika Rasi ya
Sinai tangu siku ya Ijumaa kwa amri ya Rais Abdul Fattah al Sisi wa nchi hiyo.
Kwa
miaka mingi sasa jeshi la Misri limekuwa likipambana na magenge yenye silaha
katika Peninsula ya Sinai yaliyoshadidisha mashambulizi yao tangu jeshi la nchi
hiyo lilipompindua Mohammad Morsi, rais wa kwanza kabisa kuchaguliwa
kidemokrasia nchini Misri katikati ya mwaka 2013.
MAGAIDI WASIOPUNGUA 12 WAMEUAWA NA JESHI LA MISRI KASKAZINI MWA RASI YA SINAI.
Reviewed by safina radio
on
February 12, 2018
Rating:

No comments