WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA ATAKA MASHAMBA YALIYOHIFADHIWA KWA AJILI YA MALISHO KUPIMWA.
TAREHE 08-02-2018
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh
Majaliwwa Kassim Majaliwa ametaka Mashamba yote yaliyohifadhiwa kwa ajili ya
malisho ya mifugo yaliyokuwa yanashikiliwa na NARKO chini ya Wizara ya Kilimo,
kupimwa katika vitalu vitakavyowezesha kujua idadi ya mifugo ili kuwaruhusu
wafugaji kufuga katika maeneo hayo.
Mh Majaliwa ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma
katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu ambapo alikuwa akijibu swali la mbunge wa Misenyi
Balozi Deodoras Kamala aliyetaka kujua serikali itamaliza lini migogoro kati ranchi za taifa na vijiji
vinavyoizunguka ranchi hizo kutokana na serikali kuiundia kamati ya
kushughulikia mgogoro huo.
Mh. Majaliwa amesema kuwa kutokana na wananchi wengi
kuwa na mifugo mingi huku wakikosa maeneo ya malisho, serikali imetoa utaratibu
wa mashamba yote ya ranchi za taifa-NARKO
yaliyohifadhiwa kwa ajili ya malisho ya mifugo yapimwe katika vitalu ili
wananchi wenye mifugo wapate maeneo ya kulishia mifugo yao sambamba na kuondoa
migongano kati ya wakulima na wafugaji vijijni.
Amesema kuwa Wizara ya mifugo iliunda tume kufanya
uhakiki wa maeneo ya ranchi za taifa ili kutambua wamiliki wa vitalu hivyo
vilivyopimwa, idadi ya mifugo inayotakiwa, na kufahamu kama mmiliki wa kitalu
amepata eneo hilo kihalali au vinginevyo ili kuweza kujua idadi ya maeneo
yaliyopo kwa ajili ya kuwapeleka wafugaji wakubwa kufuga katika maeneo yao.
WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA ATAKA MASHAMBA YALIYOHIFADHIWA KWA AJILI YA MALISHO KUPIMWA.
Reviewed by safina radio
on
February 08, 2018
Rating:

No comments