MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMEZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUWATAMBUA WAFANYABIASHARA WADOGO.


TAREHE 13-02-2018


Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amezitaka halmashauri zote za wilaya hapa nchini kuwatambua wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na kuwarasimisha ili wajulikane na kasha kulipa kodi kulingana na kipato chao.


Mh Suluhu ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Togwa mjini Iringa ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

Amesema kuwa halmashauri pamoja na mikoa zinatakiwa kuwarasimisha wafanyabiashara hao sambamba na kuwatengea eneo la kufanyia biashara zao litakalokuwa na miundombuinu yote ikiwemo vyoo pamoja na kuwa na sheria zao ndogondogo.

Aidha katika hatua nyingine makamu wa rais amewataka watendaji wa serikali kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji na kuwaondoa wananchi wanaofanya shughuli zao kwenye vyanzo hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhifadhi rasilimali na kukuza utalii hapa nchini.

Hata hivyo makamu wa rais yuko katika ziara ya siku tano mkoani Iringa ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMEZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUWATAMBUA WAFANYABIASHARA WADOGO. MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMEZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUWATAMBUA WAFANYABIASHARA WADOGO. Reviewed by safina radio on February 13, 2018 Rating: 5

No comments