WATU 77 WAMEUAWA NCHINI SYRIA.

TAREHE 20-02-2018


Mashambulizi makali ya jeshi la Syria katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Ghouta mashariki yamewaua raia 77, hayo ni kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binadamu, wakati majeshi ya serikali yakionekana kujitayarisha kwa mashambulizi ya ardhini.

Mashambulizi hayo yametokeawakati ambapo majeshi yanayounga mkono serikali yakitarajiwa pia kuingia katika eneo la Kaskazini linalodhibitiwa na Wakurdi kwenye mkoa wa Afrin, ili kukabiliana na mashambulizi ya Uturuki.

Ukiwa unashikiliwa na waasi tangu 2012, Ghouta imekuwa ngome ya mwisho ya upinzani mjini Damascus na rais Bashar al-Assad amepeleka wanajeshi katika jitihada za kuutwaa tena.

Shirika la uangalizi wa haki za binadamu lenye makao yake makuu mjini London limesema watoto 20 ni miongoni mwa raia 77 waliouawa.

Mkuu wa shirika hilo Rami Abdel Rahman amesema serikali inashambulia kwa mabomu mashariki mwa Ghouta kusafisha njia kwa ajili ya mashambulizi ya ardhini.








WATU 77 WAMEUAWA NCHINI SYRIA. WATU 77 WAMEUAWA NCHINI SYRIA. Reviewed by safina radio on February 20, 2018 Rating: 5

No comments